Kuhusu Sisi
Shirika la Nyumba Zanzibar ni taasisi ya Serikali inayojitegemea ambayo imeanzishwa chini ya Sheria namba 6 ya mwaka 2014. Kupitia sheria hii Shirika limepewa mamlaka ya kusimamia na kuendeleza sekta ya nyumba Zanzibar kwa lengo la kuongeza pato la Taifa na kuwapatia wananchi makaazi bora na salama.
Kabla ya kuanzishwa kwa Shirika la Nyumba mnamo Machi 2000 hadi Agosti 2015 majukumu hayo yakisimamiwa na Idara ya Nyumba (Majenzo) ambayo ilikua chini ya Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi. Hadi pale Serikali ilipoamua kufanya mageuzi ya maendeleo ya Sekta ya Makaazi na kuanzishwa rasmi kwa Shirika la Nyumba Zanzibar.
Hapo awali kazi kubwa iliyokuwa inatekelezwa na Shirika la Nyumba lilikuwa ni kusimamia na kuziendeleza Nyumba za Makaazi zilizopo Unguja (Michenzani, Kikwajuni, Kilimani, Mombasa Kongwe, Makunduchi, Gamba na Bambi) na Pemba (Madungu, Mtemani, Wete) kwa kuzikodisha, kukusanya kodi na kuzifanyia matengenezo pale inapohitajika.
Ila kuanzia 2020 Shirika lilianza shughuli za kujenga nyumba mpya za gharama nafuu na maduka kwa ajili kwa kuleta maendeleo katika Sekta ya Makaazi na lilianza na Mradi wa Mombasa Unguja na Mkungu Malofa Pemba, na kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Shirika linaendelea na miradi mengi mengine mikubwa kama vile Mradi wa Chumbuni awamu ya kwanza wenye jumla ya nyumba 1095 Mradi wa Kiembe Samaki, Mradi wa Mombasa awamu ya pili na Mradi wa Kisakasaka.
Mnamo mwaka 2024 pato la mwaka la Shirika liliongezeka kwa asilimia 100%, pamoja na kuanzishwa kwa kampuni ya Ujenzi na Ushauri Elekezi ambayo inatoa huduma kwa taasisi za Serikali na Binafsi